Yafuatayo ni mambo yanayo sababisha ukosefu wa nguvu za kiume.
MAGONJWA YANAYO SHAMBULIA MFUMO WA DAMU PAMOJA NA MISHIPA YA DAMU.
Damu ndio nishati inayo wezesha kusimama kwa uume na kuufanya kuwa mgumu na imara kama msumari. Damu ndio nishati inayoweza kuufanya uume uendelee kusimama wakati wa tendo la ndoa.
Damu ndio nishati inayo upa uume uimara na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara moja.
Hivyo basi ili uume uweze kuwa imara na wenye nguvu, pamoja na kuwa na uwezo wa kumudu na kustahimili tendo la ndoa wakati wowote , basi ni lazima mwanaume awe na mfumo imara wa damu utakaoruhusu kutiririka kwa damu kwenda katika sehemu mbalimbali za mwili ikiwamo uume.
Ili mfumo uweze kuwa imara ni lazima mhusika awe na damu ya kutosha, na pili awe na mishipa ya damu yenye afya.
Katika mwili wa mwanadamu, kuna mishipa inayo tumika kusafirisha damu kutoka katika sehemu moja ya mwili kwenda katika sehemu nyingine ya mwili ikiwemo uume. Mishipa hiyo ni kama vile vena (veins), atery ( ateri) na capillary ( kapilari ).
Mishipa hii ya damu inapaswa kuwa imara na yenye afya njema wakati wote. Mishipa hii ikipatwa na hitilifu, basi itazuia kusafirishwa kwa damu katika sehemu mbalimbali za mwili wa mwanadamu na hatimaye kufanya suala la kuwa na nguvu za kiume kwa mhusika kuwa ugumu kwa sababu ya kushindwa kupeleka damu kwenye mishipa ya uume.
Magonjwa kwenye mishipa ya damu huzuia kutirika kwa damu kwenye ogani muhimu kama vile moyo, ubongo na figo.
VIASHIRIA VYA MAGONJWA KWENYE MISHIPA YA DAMU.
Utajuaje kwamba una magonjwa kwenye mishipa yako ya damu ?
Ukiwa una matatizo yafuatayo ya kiafya, ni ishara kwamba, una magonjwa kwenye mishipa yako ya damu:
1.Kolestrol ( Ama lehemu kwenye damu )
Kolestrol nyingi kwenye damu, huzuia kutiririka kwa damu. Kolestrol ikizidi kwenye damu, hupelekea kuziba mishipa ya ateri ambayo kazi yake ni kupeleka damu kwenye uume. Matokeo yake ni mhusika kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake barabara kwa sababu uume hauwezi kusimama bila damu kuingia ndani ya mishipa ya uume. Hivyo basi pamoja na dawa ya nguvu za kiume, yakupasa kutibu kolestrol. Unaweza kuondoa kolestrol kwenye damu kwa kutumia dawa mbali za asili kama vile mdalasini,uwatu, habbat sodah etc.
1.Shinikizo Kubwa la Kupanda
Shinikizo Kuu la Damu husababisha mishipa ya ateri ambayo hutiririsha damu iingiayo kwenye uume kuziba na kushindwa kutanuka kwa kiwango inachotakiwa kutanuka.
Pia huifanya mishipa laini katika uume kushindwa ku-relax na hivyo kushindwa kuizuia mishipa ya vena ya kunyonya damu kutoka kwenye mishipa ya uume na kuipeleka kwenye maeneo mengineyo ya mwilini.
Matokeo yake kunakuwa hakuna kiasi cha kutosha cha damu iingiayo kwenye uume na hivyo kufanya uume ushindwe kusimama.
Vile vile hata kiasi kidogo cha damu kinacho ingia kwenye uume, kinashindwa kuendelea kuhifadhiwa ndani ya uume wakati uume ukiwa umesimama, na matokeo yake ni uume kusinyaa ndani ya kipindi kifupi sana tangu usimame.
Pamoja na kutumia dawa ya nguvu za kiume, unapaswa pia kutumia dawa asilia kujitibu tatizo la shinikizo kuu la damu.